Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo katika ushindi wa Real Madrid wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla katika Uefa Super
Cup siku ya Jumanne, yamemfanya mreno huyo kufikisha mabao 70 katika mashindano yote ya Ulaya na kumpita mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Ronaldo aliwai kuwa na mabao 18 nyuma ya Messi mwezi Aprili 2012, lakini akalifunga pengo hilo baada ya kufunga mabao 12 na kisha kuweka rekodi ya mabao 17 katika michezo miwili ya mwisho Ligi ya Mabingwa - na mabao yake mawili siku ya Jumanne yana maana kuwa sasa ana mabao mawili mbele ya Muargentina Messi katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote kwa wafungaji wa barani Ulaya.
Mreno huyo sasa ana mabao 68 ya Ligi ya Mabingwa na mabao mawili katika UEFA Super Cup yanamfanya kuwa na jumla ya mabao 70 na amemfikia nyota wa zamani Juventus na AC Milan Fillipo Inzaghi.
Ronaldo ni sasa anahitaji mabao sita tu kumfikia mchezaji wa zamani wa Real Madrid Raul, ambaye alifunga mabao 76 ya mashindano ya Ulaya akiwa na Real pamoja na Schalke.
wakati huo huo Messi, amefunga jumla ya mabao 68 , mabao 67 ya Ligi ya Mabingwa na moja katika UEFA Super Cup.
Kwa ujumla, Ronaldo sasa amefunga mabao 254 katika michezo 247 akiwa na Real Madrid.
0 Comments