Ibrahim Toure, ndugu na mdogo wa wachezaji wawili wa Premier League ambao kwa sasa wanaitumika timu yao
ya taifa Ivory Coast Yaya na Kolo Toure, amefariki dunia akiwa umri wa miaka 28, kwa mujibu wa chama cha soka cha nchi hiyo.
ya taifa Ivory Coast Yaya na Kolo Toure, amefariki dunia akiwa umri wa miaka 28, kwa mujibu wa chama cha soka cha nchi hiyo.
Ibrahim pia alikuwa mchezaji wa kandanda,na alicheza kama mshambuliaji katika klabu ya Misri Misr El-Maqasah na ya Lebanon ya Al Safa.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, na chama cha soka chaIvory Coast kiliahidi kutoa support kwa familia Toure.
Taarifa ilisomeka: "Kolo na Yaya Toure wanasikitika kwa kifo cha ndugu yao, Toure Oyala Ibrahim. Ivory Coast yote tunatoa ujumbe kuonyesha support kama wachezaji".
Rais wa FIFA Sepp Blatter alitumia mitandao wa kijamiiwa Twitter kutoa salamu zake za rambirambi
Aliandika: "nimefadhaishwa sana na kifo cha Oyala Ibrahim Touré, ndugu mdogo wa Yaya & Kolo Toure salamu zangu za rambirambi kumpoteza RIP..."
sababu ya kifo cha Ibrahim azijathibitisha lakini taarifa zilizoenea zinasema kijana huyo amekuwa akipatiwa matibabu ya kansa katika mji wa Manchester.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments