Herman Kihwili
IMEWEKWA.Jun. 20,2014 SAA 11:40 JIONI
Kocha mkuu wa Hispania Vicente del Bosque anakubali kuwa hakuweza kutoa hudhuru yeyote baada ya timu yake
kupoteza mchezo kwa mabao 2-0 dhidi ya Chile, na kufanya timu hiyo kupoteza matumaini yao ya kubaki Kombe la Dunia.
Baada ya kufungwa mabao 5-1 na Uholanzi katika mechi yao ya ufunguzi, del Bosque alikuwa na matumaini ya kutosha katika mchezo wa jana, lakini badala yake aliona matumaini yanateketea kwa timu hiyo ya Group B na hatimaye kushindwa.
" hatuna udhuru," alisema del Bosque.
"Tulikuwa polepole mno, tulikosa kujiamini tangu mwanzo, leo ni siku ya huzuni kwa wachezaji wote na ni muda wa kufikiria siku zijazo"..
"Tuliicheza michezo miwili, na hatukuweza kuwa bora kuliko Uholanzi au Chile, hivyo tumetolewa nje ya Kombe la Dunia".
"Tulidhani tulikuwa na nafasi nzuri sana, wachezaji bora. Lakini ukweli ni tulikuwa tofauti. "
Kipa na nahodha Iker Casillas aliongeza: "Ni vigumu kueleza kile kilichotokea mimi naomba msamaha, Tulijitahidi na hatukutaka kuwakatisha tamaa watu"...
Iker Casillas pia anaamini sasa ni wakati wa kuangalia siku zijazo,na kufikiri juu ya mchezo ujao na kitahidi kuwa bora.lakini pia amekili kuwa Uholanzi na Chile walikuwa bora kuliko Hispania.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments