Winga wa England Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa nje katika mchezo wa leo Alhamisi wa Group D dhidi ya timu ya
Uruguay.
Mchezaji huyo wa Arsenal amerudi katika mazoezi ya wiki hii baada ya kujeruhiwa katika mishipa ya goti katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Dunia kati yao na Ecuador.
Hata hivyo, meneja Roy Hodgson anatarajia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuwa atapatikana katika kikosi cha England katika mchezo dhidi ya Costa Rica.
0 Comments