Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA MPYA KUTOKA YANGA KUHUSIANA NA TAWI LA TANDALE

IMEWEKWA.May. 23,2014 SAA 10:36 ALASIRI
Uongozi wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye mojawapo ya vyombo vya
habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.

Mnamo Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.

Kufutwa kwa Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya wanachama mia moja (100)  kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC, Ibara ya 6, kipengele cha 4 "Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya wanachama ambao wanaweza kunda tawi kisipungue watu mia moja (100)".

Ibara ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za uanachama kwa muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na Kamati ya Utendaji"

Baadhi ya Wanachama  walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja anajifuta uanachama wake.

Isiaka Dude (katikati) mmoja wa waliokuwa wanachama wa yanga katika tawi la Tandale tawi lilifutwa na uongozi wa yanga
Hivyo Uongozi wa klabu ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote watambue kuwa Tawi la Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku wanachama wengine sita  wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Mwisho wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama mapema kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa marekebisho ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay Juni Mosi 2014.

Beno Njovu
Katibu Mkuu - Yanga SC
Mei 23, 2014
Kutoka kushoto:Hamisi Matandula na Nasra Mbwana anayezungumza (hapo chini)

KAMA HAUKUSIKIA WALICHOKISEMA WANACHAMA HAO BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Post a Comment

0 Comments