Paris St Germain wako katika mazungumzo na mchezaji wa Chelsea David Luiz na wako tayari kutoa kiasi pauni
milioni 50.
Uhamisho, kama utafanikiwa, utamfanya mlinzi huyo wa Brazil kuwa beki ghali zaidi duniani.
Luiz inaonekana kuwa ameona kuwa hana mahitaji ziada na bosi Chelsea Jose Mourinho.
Nahodha John Terry amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja , na Gary Cahill yuko katika mikakati ya baadaye ya timu ya Chelsea.
Luiz alijiunga na Chelsea mwaka 2011, wakati wa uhamisho wa dirisha la mwezi Januari.
0 Comments