Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 28,2014 SAA 09:22 ALFAJIRI
Dani Alves amejibu majaribio ya mashabiki kwa kuwadhihaki mashabiki hao katika mchezo ambao Barcelona waliibuka
na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Villarreal ... kwa kufurahia ndizi iliyorushwa na mashabiki hao kwa kuitafuna katika uwanja wa Estadio El Madrigal.
Ndizi hiyo alitupwa juu ya uwanja wakati mlinzi huyo kutoka wa Brazil akiwa tayari kuchonga kona.
Lakini, badala ya kuruhusiwa kupiga kona, Alves alitulia kwa sekunde kadhaa na kuchukua tunda hilo la bure,kisha kukukata funda moja kwa haraka na kula kabla ya kuendelea na mchezo - (na inasemekana baada ya kula ndizi (eti) alicheza katika kiwango cha juu kana kwamba ameongezeka nishati).
Alves mara nyingi amekuwa anakabiliwa na ubaguzi wa rangi na anaitwa ni mpambanaji wa ubaguzi wa rangi baada ya mchezo ambao waliopoteza mwezi Januari 2013, baada ya makundi ya mashabiki wa Real Madrid kumtukana kwa kulia kama tumbili wakati wa mechi.
Ngozi ya ndizi: Mbrazil mwenzake Neymar alionekana aliketa utani baada ya mchezo kwa kupost picha katika Instagram yake huku akila ndizi, akiambatanisha na maneno 'Sisi sote ni nyani'. |
ANGALIA VIDEO
Villarreal 2 - 3 Barcelona
NIlisema: Lionel Messi alifunga Bao la ushindi kwa Barca |
Katika mchezo huo wa jana Barcelona waliibuka na ushindi kibahati maana mabao yao mawili yalipatikana kwa njia ya wachezaji wa Villarreal kujifunga wenyewe.
Wakwanza kupata bao walikuwa ni Villareal kupitia kwa mchezaji wao Cani katika dakika ya 45,na bao la pili lilifungwa na Manuel Trigueros dakika 55.
Na mchezaji wa Villareal Gabriel Paulista akajifunga dakika ya 64 na kisha mwenzake Mateo Pablo Musacchio naye akajifunga dakika ya 77.
Lionel Messi ndiye aliyepachika bao la ushindi kwa Barcelona dakika ya 83.
Kwa matokeo hayo sasa Barcelona wamefikisha alama 84 nyuma ya alama 4 dhidi ya Atletico Madrid yenye alama 88 ambao wameibuka na ushindi wa bao 1 kwa o dhidi ya Valencia katika mchezo wao, na nafasi ya tatu ameshikilia Real Madrid kwa alama 82 .
0 Comments