IMEWEKWA March. 04,2014 SAA 09:40 ALASIRI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya
wachezaji wawili wa
kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na
Kocha Rogasian Kaijage,kufuatia kurudi kambini wakiwa wamelewa.
Kocha
Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana
na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya
marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.
Twiga
Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1
katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam
Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.
TFF
tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao
wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi
nidhamu ni kitu cha kwanza.
Twiga
Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo
itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.

0 Comments