IMEWEKWA FEB. 18,2014 SAA 10:37 JIONI
Kocha Msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa (katikati) akiagwa na wafanyakazi wa Sekretariati ya Klabu ya Young Africans tayari kwa safari ya kelekea Cairo - Misri |
Charles Boniface Mkwasa kocha msaidizi
wa Young Africans mchana huu anaondoka kuelekea jijini Cairo nchini
Misri kwenda
kushuhudia mchezo wa Fainali ya (Super Cup) Mshindi wa
Klabu Bingwa Afrika timu ya Al Ahly ya Misri dhidi ya Mabingwa wa Kombe
la Washindi Afrika timu ya CS Sfaxien ya Tunisia mchezo utakaofanyika
siku ya Alhamis katika dimba la Cairo International Stadium.
Mkwasa anandoka kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia Airline
ambapo atapitia jijini Adis Ababa kabla ya kuunganisha kuelekea Cairo
ambapo atatua Uwanja wa Ndege majira ya saa 7 usiku na kupokelewa na
wenyeji kutoka ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Misri.
Kutokana na umuhimu wa mchezo huo Uongozi
wa Young Africans kwa pamoja na Benchi la Ufundi walikaa na kukubaliana
kuwa kocha msaidizi Mkwasa aende kushuhudia mchezo huo wa fainali ambao
utaweza kusaidia kupata picha ya wapinzani Al Ahly ambao watacheza na
Young Africans mwishoni mwa mwezi huu.
Lengo la safari ni
kuweza kuwaona Al Ahly wanavyocheza katika mchezo huo wa fainali, pili
ni kujua wanayocheza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani na tatu ni
kuijua timu nzima kiufundi inachezaje.
Kwa upande wake Kocha
Mkwasa amesema anaamini ataitumia vizuri nafasi hiyo ya kuutazama mchezo
wa Super Cup kwa kuwasoma wapinzani na pindi atakaporejea atasaidiana
na kocha mkuu kuwaandaa vijana tayari kwa mchezo huo.
Mkwasa mara
baada ya kuutazama mchezo huo dhidi ya CS SFaxien siku ya Alhamis jioni
saa 11 kamili kwa saa za Afrika Mashariki atarejea nchini siku ya ijumaa
n akuungana na kikosi kwa ajili ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya
timu ya Ruvu Shooting.
Al Ahly
Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa Barani Afrika watacheza na Young
Africans Tarehe 1 Machi 2014 katika mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia
katika 16 bora kisha kurudiana jijini Cairo wiki moja baadae.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz
CHANZO:www.youngafricans.co.tz
0 Comments