IMEWEKWA FEB. 18,2014 SAA 10:47 JIONI
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameondoka leo
(Februari 17 mwaka huu) kwenye
Cairo, Misri kujitambulisha kwa uongozi wa juu
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Akiwa
Cairo, Rais Malinzi ambaye alichaguliwa Oktoba 28 mwaka jana atakutana na Rais
wa CAF, Issa Hayatou pamoja na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Hicham El Amrani.
WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA
Wachezaji watatu wanaocheza mpira wa
miguu nchini Tanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili
wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Mchezaji Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na
timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam ameombewa ITC na Chama cha
Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC
Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa
Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika
ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania itatoa ITC hizo.
0 Comments