Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 20,2014 SAA 01:20 USIKU
Uganda Cranes itakutana timu ya Zambia Chipolopolo mwezi ujao kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kujiandaa na kufuzu kwa
Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Shirikisho
la Vyama vya soka Uganda (Fufa) limethibitisha leo Alhamisi kwamba wao
wamekubaliana na wenzao wa Chama cha Soka cha Zambia (FAZ), kwa kila mmoja kufanya majaribio kabla ya kampeni hiyo.
Timu hizo mbili zitakutana Machi 5 katika uwanja waNdola uliopo Zambia,kama mchezo wa Uganda wa kujiandaa
kwa ajili ya mzunguko wote wa awali wa kufuzu Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) mwaka 2015 na Zambia kuendelea kujiweka vizuri kutokana na hatua ya
makundi mwezi septemba.
0 Comments