Ticker

6/recent/ticker-posts

TFF NA CRDB KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIKI

Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA FEB. 2,2014 SAA 07:39 USIKU
Mtaalamu wa tiketi za elektroniki kutoka CRDB alipokuwa akitoa ufafanuzi wa matumizi wa tiketi hizo
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya
Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.

Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.

Viwanja vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.

Post a Comment

0 Comments