Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA FEB. 3,2014 SAA 01:29 USIKU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo
la Mnyanjani katika Jiji la
Tanga.
Hati
hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75 Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6
ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu.
Kiwanja
hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali, kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa
miguu.
RAIS WA TFF
ATEMBELEA RUANGWA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama
cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Katika
ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi
mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na
kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya
Ruangwa.
MSHABIKI
MBARONI KWA MADAI YA TIKETI FEKI
Mshabiki
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa jana
(Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matei
Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam
amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe
akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia
Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni
imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za
nchini.
Tunatoa
mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi
mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu
zenye chapa ya TFF.
PAMBANO LA
YANGA, MBEYA CITY LAINGIZA MIL 175
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City lililofanyika
jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
175,285,000.
Watazamaji
30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama
za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja
sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo
mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh.
11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo
mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh.
2,278,400.
Uwanja
sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.
0 Comments