Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 3,2014 SAA 02:00 USIKU
Ligi kuu Tanzania bara imeendelea jana kwa mechi mbili zilizopigwa katika viwanja viwili tofauti,Yanga vs Mbeya City
wali kuwa wanakipiga katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Azam vs Kagera Sugar wao walikuwa wanakipiga katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Young
Africans wao walivunja mwiko wa timu ya Mbeya City kucheza michezo ya
Ligi bila kufungwa baada ya kuichapa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika
katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, bao pekee lilifungwa na Mrisho Ngasa dakika ya 16 ya
mchezo baada ya kugongeana vizuri na kiungo Haruna Niyonzima na David
Luhende kabla ya Ngasa kumtaza mlinda mlango wa Mbeya City David Burhani
na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka mchezo unakamilika Yanga 1 Mbeya City o.
 |
Mbeya City walipata nafasi kadhaa kushambulia lango la yanga |
 |
Mashabiki wa Yanga |
 |
Yanga tena |
 |
Mtokeo ya mwisho wa mchezo |
 |
Upande wa Mbeya City pia ulitawaliwa na jezi za rangi nyekundu |
 |
Mshangao kwa mashabiki wa yanga baada ya kukosa bao |
 |
Yanga na Mbeya City wameingiza sh.
175,285,000. |
 |
Mshabiki wa Mbeya City akiwa amezimia,kuelekea mwishoni mwa mchezo |
 |
Kocha mkuu Yanga Hans Van der Pluijm na kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa wakiwa makini kuangalia mchezo |
 |
Waamuzi wakitoka uwanjani baada ya mchezo |
 |
Kocha msaidizi wa YangaCharles Boniface Mkwasa akisalimiana na mashabiki |
 |
Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' (kushoto menye shati la kawaida ) akiwasalimia mashabiki baada ya mchezo |
 |
Athumani Iddi akiwa na Mbuyu Twite |
 |
Kocha mkuu Hans Van der Pluijm |
 |
Mbeya City kama kawaida yao walivyo maliza mchezo walipasha kidogo |
|
 |
Mbeya City wakitoka uwanjani |
 |
Shabiki aliyetokea upande waliokaa mashabiki wa Mbeya City akishangia baada ya mchezo kumalizika,na kwenda katika katika benchi la Mbeya City |
 |
Shabiki akiwa chini ya ulinzi wa polisi |
 |
Akinyoosha mikono juu iliyofungwa pingu, kuashilia kwamba anasalimu amri |
 |
Mikono juu |
 |
Kocha wa Simba SC, Zdravko Logarusic pia alikuwepo kuangalia mchezo |
 |
Shabiki akiojiwa na maafisa usalama |
 |
Mchezaji wa Yanga Shaaban Kondo(kushoto),akiwa chini ya ulinzi baada ya kutaka kwenda katika bechi la Yanga bila ya utambulisho wa aina yoyote,na polisi kumuweka chini ya ulinzi bila kumtambua kama ni mchezaji.Alipelekwa kituoni lakini leo amejiunga na kikosi hicho cha Jangwani baada ya kuachiwa huru.Kulia ni shabiki aliyetiwa nguvuni pia |
 |
Wachezaji wa Yanga wakijalibu kumtetea mchezaji mwenzao |
 |
Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto (aliyevaa begi)pia akijalibu kumtetea mchezaji huyo |
 |
Mrisho Ngasa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo |
 |
Mchezaji wa Yanga Shaaban Kondo akipelekwa kituoni |
 |
Katika uwanja wa Uhuru,wachina pia walikuwa akifanya mazoezi ya mpira hapo jana |
Mchezo mwingine wa ligi kuu Tanzania bara kwa siku ya jana Ulikuwa ni kati ya Azam Fc ambayo imepewa kibali na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF cha kuchezea mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanza unaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu,yenyewe Azam ilikuwa ina cheza na timu ya Kagera Sugar katika uwanja wao huo.
Na katika mchezo huo Azam imeibuka na ushindi wa mabao 4 kwa 0,mabao yao yaliyofungwa na Brian
Umony ambaye alifunga mabao mawili dakika ya 13 na 48, Kevin Friday
alifunga bao lake katika dakika ya 51 na Jabir Aziz yeye akapigilia
msumali wa mwisho katika dakika ya 83.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu
Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi).
0 Comments