Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA FEB. 7,2014 SAA 01:02 JIONI
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Februari 8 mwaka huu)
kwa mechi moja kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting
itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
nyingine nne za ligi hiyo zitachezwa keshokutwa (Februari 9 mwaka huu) kwenye
viwanja mbalimbali. Mgambo Shooting vs Simba (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT vs
Kagera Sugar (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers vs Coastal Union
(Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Mbeya City vs Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya).
FDL YAANZA
VUMBI LA MZUNGUKO WA PILI
Mzunguko
wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) unaanza kesho (Februari 8 mwaka huu) kwa
mechi za kundi A na B wakati kundi C lenyewe litaanza mechi zake Februari 22
mwaka huu.
Mechi
za kundi A ni Green Warriors vs Tessema (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi), Polisi
Dar es Salaam vs Transit Camp (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Februari 9
mwaka huu ni African Lyon vs Villa Squad (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi) na
Friends Rangers vs Ndanda (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam).
Kundi
B kwa kesho (Februari 8 mwaka huu) ni Polisi Morogoro vs Burkina Faso (Jamhuri,
Morogoro), Lipuli vs Mkamba Rangers (Samora, Iringa), Kurugenzi vs Kimondo
(Wambi, Mufindi) na Mlale JKT vs Majimaji (Majimaji, Songea).

0 Comments