Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:MANUEL PELLEGRINI ANAHISI WAAMUZI WALIIGHARIMU MAN CITY DHIDI YA BARCELONA

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 19,2014 SAA 11:19 JIONI

Manuel Pellegrini anaamini mwamuzi Jonas Eriksson aliyeamua mchezo wa Manchester City ambao walifungwa mabao 2-0 na
Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya,usiku wa kuamia hii leo,aliipendelea Barca mwanzo mpaka mwisho wa mchezo huo
  
City imefungwa katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora,ambapo walikuwa na matumaini ya kushinda,lakini sasa wana mlima wa kupanda dhini ya Wacatalunya hao.

Bosi huyo wa City, ambaye alimuona Dani Alves akipachika bao la pili kwa Barca katika hatua za mwisho, aliiambia Sky Sports: "Bila shaka mimi nina malalamiko, si tu kwa ajili ya adhabu na kadi nyekundu".
"Nadhani katika mechi nzima hatukuwa na mwamuzi mwenye uadilifu kwa timu zote mbili."
"Yeye aliamua mchezo. Aliamua mchezo kwa sababu kulikuwa na faulo ya (Sergio) Busquets dhidi ya Navas. Mwamuzi aliona makosa zaidi ya matatu,lakini hakupiga filimbi na baada ya faulo kutoka kwa Demichelis moja kwa moja akamtoa nje kwa kadi nyekundu,ilikuwa si adhabu"

"Makosa muhimu dhidi ya timu kubwa kufanya kama Barcelona ni vigumu kushinda."  

City sasa wanahitaji kushinda angalau mara mbili katika mchezo utakaopingwa katika uwanja wa Nou Camp March 12.

Post a Comment

0 Comments