Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIDANE AZIDI KUJIKUSANYIA MAVYETI TU,HII NDIYO DIPLOMA YAKE MPYA

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 17,2014 SAA 06:59 USIKU 

Mkongwe kutoka nchini Ufaransa  Zinedine Zidane ambaye kwa sasa anafanya kazi kama msaidizi wa kocha Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid, siku ya Alhamisi amefuzu kwa kupata
diploma katika maswala ya usimamizi wa michezo katika Kituo cha Sheria na Uchumi kwa Michezo huko Limoges.

Zidane hakutangaza habari hii yeye mwenyewe, lakini Olivier Dacourt  ambaye alikuwa mchezaji mwenzake na kiongo wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa aliweka picha katika mtandao wa Twitter akiwa na mshindi huyo wa zamani wa Ballon d'Or, wakiwa na vyeti vyao vya diploma.
Wanalingishia:doli doli!,doli samwela

"Hatimaye tumehitimu ..." aliandika Dacourt katika Twitter, ambapo mchezaji huyo katika miaka yake aliwahi kucheza mpira katika vilabu vya Uingereza na Italia. 

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya Zidane kuwa kocha katika siku zijazo, Raisi wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez aliiambia televisheni ya Ufaransa siku ya Jumatatu kuwa: "Zinedine ni sehemu ya historia ya Real na nadhani tutajivunia kama angeweza kuwa kocha siku moja."

"Zidane anafanya kazi kwa kutumia akili sana akiwa pamoja na wafanyakazi, anaelewa kila kitu."  alisema Florentino Perez

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha wa sasa wa Marseille Jose Anigo pia alipendekeza kuwa Zidane hatimaye anaweza kuwa kama kocha katika klabu za mji wake. 

Zidane aliwai kucheza katika klabu ya Cannes, Bordeaux na Juventus kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2001 na kustaafu akiwa na umri wa miaka 34 mwaka 2006. 


https://www.facebook.com/pages/Jamii-na-Michezo/628606780497865?ref=hl 

Post a Comment

0 Comments