Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 16,2014 SAA 09:45 USIKU
Mchezo wa Villarreal dhidi ya Celta Vigo ulisimamishwa kwa muda siku ya Jumamosi usiku baada ya mabomu ya machozi kutupwa juu
ya uwanja.
Wachezaji wa kutoka pande zote mbili walielekea nje ya uwanja katika hatua ya mwisho ya vurugu katika mechi hiyo ya La Liga,na Celta Vigo ilikuwa ikiongoza kwa 1-0,ambapo
vyombo vya habari vilisema mabomu ya machozi yalirushwa karibu na
lengo la timu hiyo (wageni) na kuanza kutoa nje wingu zito la moshi mweupe.
Ni wazi Wachezaji wote walikuwa katika hatari ya kuumia kutokana na athari ya gesi,
Kipa wa Celta Vigo Yoel Rodriguez ilionekana akikimbia kutokana na moshi uligubika machoni mwake.
Mashabiki walifunika nyuso zao pia walielekea nje ya uwanja.
Mechi hatimaye ikaanza tena katika uwanja mtupu na Celta ikashinda kwa mabao 2-0 kwa katika dakika ya 90.
Kushinda kwa Celta kuna maana Villarreal amekosa nafasi ya kuwa karibu na Athletic Bilbao kwa alama nne.
Zaidi ifuatavyo ..
Mashabiki wa ndani ya uwanja wa El Madrigal wakitoka nje baada yakurushwa kwa mabomu ya machozi
mwana usalama wa mechi ya Villarreal dhidi ya Celta Vigo akijaribu kujikinga na moshi wa mabomu ya machozi
Usalama kwanza:Mashabiki wakiondoka katika uwanja wa El Madrigal baada ya mabomu ya machozi kutupwa juu ya uwanja
Chungu :kipa wa Celta Yoel RodrÃguez akifunika macho yake baada ya kurushwa kwa mabomu ya machozi katika uwanja
Mshambuliaji wa Villarreal Jonathan Pereira akipiga mateke bomu la moshi lililotupwa kwenye uwanja wa El Madrigal
0 Comments