IMEWEKWA JANU. 17,2014 SAA 07:05 USIKU
Mkwasa na Wolfagang |
Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani ambao kwa sasa ni
makocha wa timu ya Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na
msaidizi wake
Wolfgang leo jioni kabla ya mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel
ya Sueno Beach na kuongea kidogo na makocha wa Young Africans Hans na
Mkwasa masuala ya kiufundi kisha kuagana nao na kuwaacha waendelee na
progam yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa miaka
nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na
kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa
ameambatana na kocha wake msaidizi Wolfagang .
Kocha Msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa akiwa na Kocha Berit Vogts |
Kocha mpya wa Young
Africans mholanzi Hans Van Der Plyum leo ameanza rasmi kazi ya kukinoa
kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara katika viwanja
vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza katika ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Hans ambaye amejiunga na
Young Africans wiki hii akichukua nafasi ya kocha mholanzi aliyeondoka
Ernie Brandts amesema atajitahid kadri ya uwezo wake pamoja na wachezaji
na benchi la ufundi kuona wanaisaidia timu kufika hatua nyingine mbele
zaidi.
"Amesema hawezi kufanya jambo lolote peke yake bali kwa
kushirikiana kwa pamoja atafanikiwa kwani katika mchezo wa jana timu
yake iliweza kucheza soka la kujituma na kushirikiana mwanzo mwisho kitu
ambacho ndio falsafa yake katika ufundishaji" alisema Hans.
Timu
ilifanya mazoezi ya asubuhi leo saa 5 kamili kwa saa za Uturuki mpaka
saa 6:30 kabla ya kupumzika na kurejea tena mazoezini jioni saa 11
kamili jioni mpaka saa 12:30 ambapo alikuwa akiwaelekeza wachezaji jinsi
gani anapendelea wacheze kwa kufuata mfumo wake.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Plyum akiwa na msaidizi wake Charles Mkwasa kabla ya kuanza mazoezi ya kuanza kwa mazoezi ya jioni katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach |
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara
baada ya mazoezi ya leo kocha Hans amesema timu ya Young Africans ina
wachezaji wazuri ambao wana uwezo binafsi na bado wana nafasi ya kucheza
soka kwa kipindi kirefu hivyo kikubwa wanapaswa kuwa fit muda wote ili
waweze kutimiza majukumu yao.
Young
Africnas itaendela na mazoezi kesho na asubuhi katika viwanja vya hotel
ya Sueno kujiweka sawa kwa mchezo utakaofuata wa kirafiki kabla ya
kurejea nchini wik ijayo tayari kwa mikikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom na
mashindano ya kimataifa.
https://www.facebook.com/pages/Jamii-na-Michezo/628606780497865?ref=hl
Chanzo:youngafricans.co.tz
0 Comments