Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA JANUARI 2.2014 SAA 8:25
Arsenal huenda ikakabiliwa na mgogoro katika safu ya ushambuliji siku ya Jumamosi katika Kombe
la FA dhidi ya wapinzani wa
Tottenham Hotspur baada ya Nicklas Bendtner
kujeruhi kifundo cha mguu wake katika mchezo wa Ligi kuu ambao waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya
Cardiff City siku ya Jumatano.Pigo: Nicklas Bendtner kaumia kifundo cha mguu wake baada ya kufunga bao la ufunguzi kwa Arsenal dhidi ya Cardiff |
Mchezaji huyo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Lukas Podolski katika nusu ya pili lakini ni baada ya kufunga bao katika dakika ya 88 .
"Kwa
bahati mbaya yeye (Bendtner) amejeruhiwa leo na inaonekana kama si
suala la siku, lakini ni wiki. Nasikitika sana kwa ajili
yetu,na kwa ajili yake pia," Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
aliwaambia waandishi wa habari.
Kidonda kimoja: Bendtner kaumia kifundo cha mguu katika mgongano na kipa David Marshall baada ya kufunga bao kwa Arsenal |
Ushindi wao ilikamilishwa na Theo Walcott katika uwanja wa Emirates na kuwafanya Arsenal kuwa na hatua moja juu Man City.
0 Comments