Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA DISEMBA 20,2013 SAA 03:01 USIKU
Boniface Wambura Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
|
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya
matumizi ya tiketi za
elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi,
Dar es Salaam.
Mechi
ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo
itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa
Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.
TFF
tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali
ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za
elektroniki unavyofanya kazi.
Kwa
kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya
tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine
majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
0 Comments