Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 8.2013 SAA 08:21 USIKU
Arsene Wenger amekubali kuwa anajisikia tofauti(vigumu) kwa yeye kumuona Robin van Persie akiwa amevaa shati nyingine
yoyote zaidi ya Arsenal.
Wenger
atakutana na MDutchman huyo kwa mara nyingine tena siku ya Jumapili,ambapo timu hiyo inayoongoza Ligi
Kuu itakutana na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.
Ingawa
ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kumuuzwa Van Persie kwa Sir Alex
Ferguson kwa 24million £, Wenger anasema hawezi kukaa vizuri akimuona mshambuliaji huyo katika kikosi cha United.
Msimu wa kwanza wa Van
Persie uliomalizika ndani ya Old Trafford,aliweza kuipatia ubingwa wa kwanza
wa Ligi Kuu', miaka nane baada ya Wenger kumpeleka England
kutoka Feyenoord.
"Bila shaka ni ajabu kwa sababu kwangu mimi, yeye ni mtu wa Arsenal," Wenger alisema.
"Mimi nilimchukua yeye wakati alikuwa mchezaji kijana sana,tulikuwa pamoja katika njia ya vipindi vigumu sana. Na akawa mchezaji wa daraja la
dunia, kwangu mimi yeye ni mchezaji wa Arsenal."
Wenger
pia umebaini kuwa ni kocha wa zamani msaidizi wa United Rene Meulensteen,ndiye aliyeshawishi van Persie kujiunga na kikosi hiko cha united.
"Robin
van Persie alikuwa ameshawishika na kocha wa Kiholanzi ambaye alikuwa
katika klabu ya Manchester United sasa anafundisha Anzhi Makhachkala, (hivyo) kwamba alicheza sehemu kubwa ya uhamisho wa mchezaji huyu," Wenger
alisema.

0 Comments