Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOVEMBA 20.2013 SAA 01:40 USIKU
Waathirika
wa mabomu Mbagala yaliyolipuka mnamo tarehe 29/04/2009 wamemtaka naibu
mkurugenzi wa maafa hayo Mama
Nanai kutowaingilia katika madai yao kwani wanasubiri
uamuzi utakaotoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Jakaya
Mrisho Kikwete.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es salam mwenyekiti wa waathirika wa mabomu hayo Bw
Steven Gimonge amedai kuwa naibu mkurugenzi huyo ambaye amehamishia ofisi zake
katika majengo ya ofisi ya Kata Mbagala
kuu katika manispaa ya Temeke jijini Dar es salam asimshinikize Raisi kutoa maamuzi kwani
amekuwa kero kwa waathirika hao.
“Tunayo
hakika kwamba Naibu Mkurugenzi hana nafasi kwa kipindi hiki maana tatizo letu halipo
ofisini kwake tatizo letu tumeshalifikisha kwa Muheshimiwa Raisi na tuna hakika
hawezi kumtumia yeye(naibu mkurugenzi) katika kumaliza tatizo hilo”alisema Bw
Gimonge .
Aidha Bw
Gimonge amemtuhumu Naibu Mkurugenzi huyo pamoja na watumishi wengine kwa kufanya
ufisadi wa kuchukuwa haki yao na kuwalipa waathirika hao Sh 1,400 na 1,950 za
kitanzania na kuwataka wawe na subira mpaka hapo uamuzi huo utakapopatikana.
Ikiwa ni
takribani miaka minne tangu maafa hayo kutokea na kusababisha baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kupoteza
maisha pamoja na mali zao,bado serikali haijawa na kauli thabiti kuhusu kulipwa
fidia kwa waathirika hao jambo ambalo linawaweka katika wakati mgumu wananchi
hao wakiwemo wazee,wanawake pamoja na watoto .
0 Comments