Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 21.2013 SAA 6:50 USIKU
Klabu ya West
Brom wameombwa msamaha kutoka kwa mkuu wa Mwamuzi 'Mike Riley kufuatia penalti waliopewa Chelsea katika
muda wa majeruhi katika uwanja wa Stamford
Bridge mapema mwezi huu.
Albion walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1 hadi mwamuzi Andre Marriner kufanya maamuzi yenye utata dakika kadhaa kabla ya mchezo kumalizika kufuatia changamoto kati ya mchezaji wa West Browm Steven Reid na Ramires.
Eden Hazard alifunga penalti na kupata sare ya mabao 2-2, na kuwanyima West Browm ushindi wa kwanza wa ligi wa kushinda katika uwanja wa Stamford Bridge tangu 1978.
"Tumekuwa na simu kutoka kwa Mike Riley ya kuomba msamaha," alisema bosi Steve Clarke.
"Yeye ni wazi alifanya uamuzi ambao sio sahihi,hatuwezi kupata pointi yeyote zaidi, Lakini ni vizuri kwa Mike kutupigia simu."
Majibu kutoka kwa
Riley ambaye ni Mkuu wa michezo na kiongozi wa mechi,ni wazi yako kinyume moja kwa moja na utetezi wa kocha wa Chelsea Jose Mourinho' baada ya mechi ambapo alitetea uamuzi wa refa Andre Marriner .
"nimeangali mara mbili au tatu na ilikuwa ni adhabu ya wazi kabisa ," Mourinho aliiambia BBC Sport. "Mwamuzi alifanya makosa mengi wakati wa mchezo lakini haikuwa ni makosa."
Riley alipiga simu katika klabu ya West Browm nakuomba msamaha mara mbili ndani ya mwezi,
na mwamuzi wa zamani wa fainali za Kombe la Dunia Howard Webb pia
alisema pole adhabu na kusababisha kutoka sare.
Klabu ya West Blowm imetuma barua kwa uongozi unaosimamia ligi kuu na kwa jopo la waamuzi (PGMOL ) wakielezea maamuzi ya adhabu nne ambazo zimekwenda dhidi yao katika michezo 11 ya ufunguzi wa msimu.
0 Comments