Ticker

6/recent/ticker-posts

UMESIKA ALICHOKISEMA ZLATAN IBRAHIMOVIC BAADA YA KUKOSA KWENDA BRAZIL?...(ukishasoma toa maoni yako kama ni kweli au la)

Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 21.2013 SAA 8:10 USIKU
Mshambuliaji  wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amedai kuwa Kombe la Dunia litakuwa halina  thamani ya kuangalia bila kuwepo yeye,baada ya
timu yake kutolewa na Ureno siku ya Jumanne usiku katika mechi ya kufuzu kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Ibrahimovic alifunga mara mbili lakini utendaji wake kazi haukufua dafu mbele ya Cristiano Ronaldo katika vita kati yao, kufuatia Mreno huyo kushinda mara tatu katika ushindi wa mabao 3-2, na kuwa jumla ya mabao 4-2.
kwa miaka yake 32, inaonekana Ibrahimovic ni mwisho wa nafasi yake ya kucheza kwenye hatua ya dunia sasa umepita. 

"Ni jaribio la mwisho pengine kufikia Kombe la Dunia na timu ya taifa kwangu ," alisema kwa mipango yake, Zlatan  na kuongeza. "Jambo moja la uhakika, Kombe la Dunia bila mimi,hakuna kitu cha kuangalia, hivyo si vyema kusubiri Kombe la Dunia". alisema  Zlatan Ibrahimovic

"Hongera kwa Ureno lakini timu zote mbili zilistahili kucheza Kombe la Dunia.aliongezea tena Zlatan.
"Tunajisikia vibaya kiukweli  kwa sasa,Kombe la Dunia nchini Brazil itabaki ndoto kwa timu ya taifa ya Sweden"alimalizia Zlatan Ibrahimovic.

Ni wakati wa nyota wa Real Madrid tena kuiwezesha Ureno kupitia. 
Baada ya mechi, Ronaldo alisisitiza hakuweza kuchukuwa motisha yeyote  kutokana hofu ya Ibrahimovic,nakusema ni malengo na  tamaa yake mwenyewe ya kufikia fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil. 
"Mimi si kushindana dhidi ya Zlatan, yeye ni mchezaji wa ajabu na nyota mkubwa nchini Sweden, lakini mimi sikushindana dhidi yake," Ronaldo alisema. 

  "Mimi nilicheza kwa ajili ya timu yangu." 

"Sasa timu imepongezwa,kitu gani tulitaka kitimie, Sasa tunasubiri  na kufurahia. Tunaweza kurudi katika klabu zetu kwa dhamiri safi, kufanya kuwe na msimu mkubwa na kisha kuangalia mbele kwa ajili ya Kombe la Dunia"alimalizia kusema Cristiano Ronaldo. 


UNARUHUSIWA KUSHARE STORY HII KWA MARAFIKI ZAKO 

Post a Comment

0 Comments