IMEWEKWA NOVEMBA 5.2013 SAA 10:11 JIONI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa
miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya
wote
waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
Oktoba
28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi,
Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa
sababu mbalimbali.
Hata
hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa
au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
Vyama
vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao
(vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote
waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).
0 Comments