Ticker

6/recent/ticker-posts

ROBINHO AITWA KATIKA KIKOSI CHA BRAZIL

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 31,2013 SAA 5:24 USIKU
Mchezaji wa klabu ya AC Milan  Robinho amekuwa surprise siku ya Alhamisi kwa kuchaguliwa na kocha Luiz Felipe Scolari na kuitwa katika kikosi cha  Brazil kitakachokutana na  Honduras na
Chile katika mechi ya  kirafiki mwezi ujao.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, ambaye alifunga mabao 28 katika michezo 84 akiwa na Brazil, ana kumbukumbu ya kukosekana kwa miaka miwili na kusafiri Amerika ya Kaskazini kwa ajili ya mechi mbili za taifa lake lakini sasa amerudi na kuendelea kukijenga kikosi chao kwa ajili ya kombe la dunia 2014 .

"Yeye anaweza kuwa namba 9, namba 7, namba 11 - Robinho ni hodari na yeye ni bora katika nafasi yoyote," Scolari aliwaambia waandishi wa habari. 
"Yeye ni hodari na mimi nataka awe hodari kwa upande wa kitaifa,natarajia kumuona ndani yake kuna nini ambacho sisi tunatakiwa  kujua kwake yeye na ubora wake wa kiufundi pamoja na  furaha.. Ni muhimu sisi kumpa nafasi ya kuona kama anaweza kuunganisha kwa pamoja  timu na ubora tunaoutaka. " 
Robinho amerejea katika fomu yake ya zamani katika msimu huu na ingawa ana mabao matatu katika mechi 13 akiwa na Milan,kwa upande wa kucheza amekuwa vizuri.
 
Winga wa Chelsea WILLIAN na beki wa kati kutoka klabu ya  Paris St Germain Marquinhos mwenye umri wa miaka  19   pia wameitwa katika kikosi lakini kiungo wa Tottenham Hotspur Sandro amebaki nje baada tu ya kurudi Ligi Kuu na hatua baada ya kuumia.
 
Kaka, ambaye pia imeonyesha ishara ya kurudi na kuunda AC Milan,pia hayupo katika kikosi kilichoitwa.
Scolari ameita  hadi wachezaji 22, wawili tu ambao hucheza soka yao nchini Brazil.
Pamoja na michuano ya ndani katika wiki yake ya mwisho, kocha alisema makusudi yake ni kuepukwa kuchukua wachezaji wengi mno kutoka klabu ndogo za mitaa.
Kipa  wa Atletico Mineiro, Victor ataanza mchezo wa kwanza dhidi ya Honduras, alisema Scolari.
Brazil atakutana na Honduras huko Miami Novemba 16 kabla ya kukutana na Chile huko Toronto siku tatu baadaye.

Kikosi:
Makipa: Julio Cesar, Victor
Walinzi: Thiago Silva, Dante, David Luiz, Marquinhos, Daniel Alves, Maicon, Marcelo, Maxwell
Midfielders: Lucas Leiva, Hernanes, Luiz Gustavo, Paulinho, Ramires, Oscar
Washambuliaji: Neymar, Bernard, Hulk, Robinho Jo
 
 

Post a Comment

0 Comments