Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England Chelsea imetangaza siku ya Alhamisi kwamba wamemsaini kijana mwenye umri wa miaka 18
kutoka katika timu ya taifa ya Burkina Faso kiungo Bertrand Traore kwa mkataba wa
miaka minne.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Burkinabe amewasili katika Chama Jeunes Espoirs De Bobo-Dioulasso, alitumia muda wake na Chelsea wakati wa ziara yao ya msimu Asia mwaka
huu,hasa baada ya kufunga mabao katika mechi dhidi ya Malaysia na Indonesia.
"Chelsea Football Club ina furaha kutangaza makubaliano kwa kumsaini Bertrand Traore," ilisema taarifa kwenye tovuti ya Chelsea. "mchezaji huyo mwenye umri wa miaka18, imekubali mkataba wa miaka minne na nusu."
Traore alijiunga na kikosi cha Burkina Faso tarehe 16 Septemba 2011 siku chache kabla ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Amecheza mechi za kimataifa 10,na kufunga bao moja.

0 Comments