Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA UJERUMANI,SASA NI ZAMU YA GOOGLE NA YAHOO KUDUKULIWA NA MAREKANI

IMEWEKWA OKTOBA 31,2013 SAA 1:50 USIKU
Nembo ya Google mojawapo ya kampuni kuu za mitandao duniani.
Kashfa ya upelelezi wa shirika hilo la usalama wa taifa la Marekani, NSA, inazidi kutapakaa baada ya kubainika kwamba imekuwa
ikidukiza mawasiliano makuu yenye kuunganisha vituo vya data vya kampuni za mitandao za Yahoo na Google duniani kote.
Gazeti la Washington Post limeripoti hapo jana kwamba taarifa za siri za tarehe 9 Januari mwaka 2013 zimedokeza kwamba NSA imekuwa ikituma rekodi za mamilioni ya mawasiliano kila siku kutoka mitandao ya ndani ya Yahoo na Google kwenda kwenye ghala ya data katika makao makuu ya shirika hilo yaliyoko Fort Meade, Maryland mjini Washington, Marekani.
Nembo ya gazeti mashuhuri la Marekani la Washington Post.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Washington Post katika kipindi cha siku 30 zilizopita wakusanyaji wa data wameshughulikia na kutuma zaidi ya rekodi mpya za mawasiliano 180 milioni kuanzia za "metadata" ambazo zingelidokeza nani aliyetuma baruwa pepe na wakati gani na maudhui yake yawe katika maandishi, sauti na video.
Kufichuliwa kwa taarifa hizo kumepokelewa kwa ghadhabu na kampuni ya Google na kuzusha masuala ya kisheria ikiwa ni pamoja na iwapo shirika hilo la NSA yumkini likawa linakiuka sheria za nchi taifa kuhusu udukuzi wa mawasiliano.

Mwandishi:Mohamed Dahman/AP

Post a Comment

0 Comments