Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZEE WA YANGA WASEMA HAWAMTAMBUI KATIBU MPYA

IMEWEKWA SEPT 4,2013 SAA 11:40 JIONI
Kamati ya baraza la wazee wa Yanga wamesema kuwa hawamtambui katibu mpya aliyeletwa katika klabu hiyo hapo jana.
Katibu wa baraza la wazee Ibrahim Akilimali amesema kuwa katibu huyo aliyekabidhiwa mikoba ya katibu wa zamani Lawrence Mwalusako amesema amekuja bila taarifa na hawaelewi amekuja

kufanya nini.
Amehoji kuwa katibu huyo amekuja bila kufuata katiba anafanyaje kazi bila kupeleka hata CV.
Katibu huyo mkenya anayejulikana kwa jina la Patrick Nagi amekuja jana na ameletwa na mtu asiyejulikana.

Post a Comment

0 Comments