Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 4,2013 SAA 10:40 USIKU
Hakika ulimwengu mzima sasa wa wapenda mchezo wa soka unajua kuwa Gareth Bale ni mchezaji wa timu ya Real Madrid,na hiyo ni baada ya kuweka rekodi ya dunia kwa kusaini kwa kitita cha pauni milioni 86 akitokea katika klabu ya Tottenham.
Hakika ulimwengu mzima sasa wa wapenda mchezo wa soka unajua kuwa Gareth Bale ni mchezaji wa timu ya Real Madrid,na hiyo ni baada ya kuweka rekodi ya dunia kwa kusaini kwa kitita cha pauni milioni 86 akitokea katika klabu ya Tottenham.
Bale ambaye amepewa jezi namba 11, baada ya kusaini mkataba wa miaka 6 ya kuichezea klabu ya Real Madrid,alitambulishwa
rasmi kwa mashabiki zaidi ya 20,000 waliohudhulia halfa hiyo.
Gareth Bale alisema najivunia sana kujiunga na Real Madrid.Aliongea kwa lugha ya kihiSpania"ni ndoto yangu kucheza katika klabu ya Real Madrid,asanteni kwa kunikaribisha. Hala Madrid! aliyasema hayo mbele ya watu zaidi ya 20,000 walioudhulia kukaribishwa kwake.
Baada ya hapo akafanya mkutano na waandishi wa habari,na kusema yuko katika klabu ya Real Madrid kwa hali yeyote ile,iwe shida au karaha.Bale alisema"uhamisho huu hauna madhara yeyote kwangu mimi,kila kitu ni juu ya Madrid na Spurs,kwangu mimi ni kuongeza nguvu ya kile ninachotaka kufanya"
Gareth Bale pia aliulizwa swala la Cristiano Ronardo kuwa katika klabu ya Real Madrid,kuwa ni moja ya sababu ya yeye kusaini katika klabu hiyo? na alikuwa na haya ya kusema "Kwangu mimi Cristiano
Ronaldo ni Boss,ni mchezaji bora wa dunia" Bale aliongeza"ninaheshimu kuwa kucheza karibu naye"
"Ninahitaji kushinda ligi ya mabingwa nikiwa na Real.malengo yangu makubwa ni kuisaidia Madrid kushinda vikombe vyote.Nahitaji kushinda vikombe vya dhahabu hapa na kuisaidia klabu hii kushinda ligi ya mabingwa..
http://www.marca.com/videosmarca/?v=CLTtrPoBYVs
MAHOJIANO MENGINE BONYEZA HIYO VIDEO HAPO CHINI

0 Comments