Ticker

6/recent/ticker-posts

LUIS SUAREZ:NINAFURAHA KUWA NA LIVERPOOL

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 4,2013 SAA 8:20 USIKU
Baada ya miezi miwili ya muingiliano na migogoro na klabu yake, tetesi za usajili na kutoeleweka juu ya hatma yake na Liverpool,hatimaye mchezaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suárez,ameweka kila kitu sawa na klabu yake hapo jana.
"Nimechagua kukaa na Liverpool tangu wiki iliyyopita"alisema mchezaji huyo wakimataifa wa Uruguay.
Luis Suarez ambaye aliripotiwa kuambiwa na kocha wake  Brendan Rodgers kufanya mazoezi peke yake baada ya migogoro kadhaa na
klabu yake,anatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu yake baada ya adhabu aliyopewa ya kumuuma meno mchezaji wa Chelsea  Branislav Ivanovic kumalizika.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa aeleweki ,mara nje mara ndani,lakini sasa ameonyesha dhamira yake ya kuwa wa timu hiyo"vyovyote  vile kama mimi kucheza au la ndani ya klabu yangu, waandishi wa habari daima hawataisha  kuzungumza juu yangu,lakini Kwa sasa wanaweza kuweka kuniweka katika  kila tumu" alisema Luis Suárez

Post a Comment

0 Comments