Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMA SOKA LA TZ LIMETUSHINDA,BASI TUJARIBU NA HUKU

IMEWEKWA SEPT 4 ,2013 SAA 7:20 USIKU
Timu ya taifa ya wanawake ya  mpira wa magongo,inatarajia kuelekea jijiji Nairobi nchini Kenya,kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 25 mpaka Oktoba 5 mwaka huu.
katibu mkuu wa chama cha mpira wa magongo mkoa wa Dar es salaam(DRHA)
Mnonda Magani
Akizungumza na Jamii na Michezo katibu mkuu wa chama cha mpira wa magongo mkoa wa Dar es salaam(DRHA),ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya mpira wa magongo,Mnonda Magani,amesema kimchezo timu hiyo iko katika hali nzuri,na kama wakipata nafasi ya kufuzu katika mashindano hayo,wataweza
kushiriki moja kwa moja katika mashindano dunia ya mchezo wa mpira wa magongo.
Timu ya taifa ya mpira wa magongo kwa wanawake,ikifanya mazoezi na timu ya magereza ya wanaume katikan uwanja wa karume jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika.
Aidha Magani ameongeza kuwa timu hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa,posho na hata sehemu ya kuweka kambi kwa wachezaji,na kuwataka wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza na kuwasaidia kwa mahitajia hayo.
Lakini pia Magani ameishukuru kampuni ya inayotengeneza soda aina ya pepsi,kwa kuwapatia shilingi milioni 3  na kuwataka wadau wengine wajitokeze ili kuwaunga mkono.
kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa magongo, Valentina Quaranta
Kwa upande wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa magongo, Valentina Quaranta ambaye amekuwa akipata msaada wa viatu kwa marafiki zake kutoka ujerumani,amesema timu hiyo iko katika hari nzuri kimchezo,kwa sababu wanafanya mazoezi ya kuwajega wachezaji wake  kiakili na kimchezo pia.
Timu iko kamili kiakili na kimchezo


Post a Comment

0 Comments