Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 24,2013 SAA 3:35 USIKU
Winga wa klabu ya Arsenal Theo Walcott atakuwa nje katika mechi mbili za timu yake ya taifa la England katika mechi za kufuzu
Kombe la Dunia kwa sababu anahitaji matibabu kwa ajili ya
maumivu ya
tumbo,hayo yamesemwa na uongozi wa klabu yake hiyo inayoshiriki ligi kuu.
"Atakuwa anatibiwa nchini Ujerumani siku ya Jumatano na, kwa sababu hiyo, tunaweza kuanza Rehab kwa ajili yake mara moja," Meneja wa Arsenal, Arsene
Wenger aliiambia tovuti ya klabu (www.arsenalcom)
"Sisi tunamatumaini ya kushughulikia swala hili kwa haraka na yeye lazima atakosa mechi nyingi za Arsenal Lakini pia atakosa michi zijazo za kimataifa na
Uingereza."
Uingereza,wako juu ya pointi
moja kwa timu ya Ukraine na Montenegro katika kundi H, ni
kutokana na kucheza na timu ya Montenegro na Poland wakiwa nyumbani Oktoba 11 na 15 katika michezo yao ya mwisho ya kufuzu kwa ajili ya mashindano ya
mwaka ujao nchini Brazil.
Walcott
amekosa ushindi wa Arsenal dhidi ya Stoke City Jumapili,ushindi uliowaweka juu
Gunners katika Ligi Kuu baada ya mchezaji huyo kupata matitizo hayo ya ukuta wake wa nyuma ya tumbo.
"Siyo ngiri, lakini inafanana kidogo kimuundo na tatizo hilo katika tumbo lake," alisema Wenger.

0 Comments