Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 25,2013 SAA 7:25 USIKU
![]() |
| Edin Dzeko akipachika bao la kwanza |
Manchester
City wamepata kulipiza kisasi kwa kushindwa kwao katika fainali za kombe la FA msimu uliopita baada ya kupata
ushindi mkubwa katika kombe la Capita one katika mchuano wao dhidi ya ushindi Wigan usiku wa jana.![]() |
| Jovetic ulifunga bao lake la kwanza dakika ya 60 kwa klabu yake tangu atie saini katika majira ya joto,kabla ya kufunga bao lingine katika dakika ya 83 |
Baada ya Edin Dzeko kutupia bao lake katika dakika ya 33,Stevan Jovetic alipachika bao lake la kwanza katika dakika ya 60 ya kipindi cha pili,kisha ikafuata zamu ya Yaya Touré ambaye alipata bao lake katika dakika ya 76,Jovetic alitumbukia tena katika nyavu ndani ya dakika ya 83 kisha dakika tatu baadaye Jesus Navas akafunga kitabu cha mabao cha Manchester City kwa ushindi huo wa mabao 5 kwa 0 dhidi ya Wigan.
![]() |
| Kuchanganyikiwa: Lopes akijilaumu baada kukosa nafasi |
Kikosi cha Manchester City: Pantilimon,
Richards, Lescott, Clichy, Boyata, Milner, Garcia, Fernandinho (Toure,
46), Lopes (Navas, 71), Dzeko (Negredo, 79) , Jovetic
Akiba wasiotumika : Wright, Kolarov, Nastasic, Nasri
Wafungaji: Dzeko 33, Jovetic 60, Toure 76
Kikosi cha Wigan:
Nicholls, Crainey (Redmond, 68), Rogne, Boyce, Barnett (Shotton, 59),
McCann, Gomez, Espinoza, Fyvie, Garcia, Dicko (Powell, 80)
Akiba wasiotumika : Carson, Buxton, McClean, McArthur
Kadi za njano: Barnett, Fyvie



0 Comments