Ticker

6/recent/ticker-posts

PHILIPPE COUTINHO ANAMATUMAINI YA KURUDI LIVERPOOL HARAKA IWEZEKANAVYO

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 24,2013 SAA 11:25 ALFAJIRI
kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho amasema amepata nafuu katika  bega lake alilofanyiwa upasuaji  na ana matumaini kurudi....
uwanjani  na kucheza hivi karibuni.
Coutinho alijeruhiwa mapema mwezi huu katika mechi dhidi ya Swansea na alihitajika kufanyiwa  operesheni kwa ajili ya kutuliza maumivu ya bega lake.
Lakini Coutinho amesema anafanya kila kitu anachoweza ili aweze kurudi  kucheza haraka iwezekanavyo - lakini awali Liverpool walithibitisha Philippe Coutinho atakuwa  nje mpaka mwishoni mwa mwezi Oktoba baada ya kuumia bega lake.
"Nimekerwa  kupata majeraha, hasa wakati nikiwa nacheza vizuri , lakini ndio hivyo imetokea," Globo Esporte  walimnukuu Coutinho akisema.
"Mimi sasa nataka kuzingatia nafuu yangu na kufanya kila kitu sahihi kuweza kurudi kwa haraka iwezekanavyo ili kusaidia Liverpool katika ligi. 
"Upasuaji ulikuwa na mafanikio, na hili ndilo jambo zuri sana, nitarudi hivi karibuni"
Coutinho yuko katika   sehemu ya kikosi cha Brazil katika kombe la  Dunia  mwaka ujao, na ana matumaini ya kushiriki  mashindano hayo  katika nchi yake.
"ndoto yangu kupata kuitwa tena kwa ajili ya kuisaidia  timu ya taifa, lakini siko peke yangu," alisema. 
"Bila shaka ni mbaya kupata majeraha  katika wakati kama huu, lakini hii ni soka"
"Nimekuwa  nikikaa nje,na kujishughulisha kwangu  tayari kumenifanya kuwa mkamilifu kwa haraka na  imewezekana, Kama nitacheza vizuri, mambo yatakuwa kawaida." alimalizia mchezaji huyo.

Post a Comment

0 Comments