Na.Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT. 25,2013 SAA 3:31USIKU
![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akizungumza hii leo |
Mamlaka ya Majisafi na majitaka Jijini Dar es
Salaam,-DAWASA, leo imetoa mapendekezo kuhusiana na maombi ya
kurekebisha bei za maji.
Akizungumza katika mkutano wa DAWASA, Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amesema
kuwa, bei ya maji itapanda
iwapo tu wananchi na mamlaka husika watakubaliana katika mkutano huo.![]() |
| Lakini pia Said Meck Sadiki alilalamika kwamba mkutano hakukuwa na wanachi wengi waliohudhulia katika mkutano huo,(lakili bei ikipanda wao ndio wakwanza kulalamika) |
Aidha Sadiki ameongeza kuwa, Serikali imekuwa ikipata lawama kutokaa na
baadhi ya watu kuharibu miundo mbinu ya maji na amewataka watu hao
kuacha kufanya hivyo kwani sheria itafuata mkondo wake.
![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiondoka baada ya kuhutumia katika mkutano huo |
DAWASA imeamua kuandaa mkutano huo ili kupata maoni ya wananchi kwani
kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya mapato ya kuweza kumudu gharama za
uzalishaji na usambazaji.
DAWASA ambayo ilianzaisha Tarehe 4/4/ 1997 na baada ya kuunganishwa NUWA na DSSA,lakini sheria ililekebishwa mwaka 1999 kuruhusu ubinafsishaji washunguli za DAWASA,na mikoa inayohudumiwa na DAWASA ni pamoja na Bagamoyo,Kibaha na Dar es saalam.



0 Comments