Ticker

6/recent/ticker-posts

HOFU YA MASHINDANO YA MAGONGO KENYA KWA TIMU YA TANZANIA

 IMEWEKWA SEPT 25,2013 SAA 1:25 USIKU
Timu ya taifa ya mpira wa magongo kwa wanawake,ilipokuwa ikifanya mazoezi na timu ya magereza ya wanaume katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika.picha imepigwa SEPT 4.
Mashindano ya mpira wa magongo kwa mataifa ya Afrika yaliyopangiwa kuanza Alhamisi wiki hii na kusogezwa mbele hadi tarehe 1 Octoba mjini Nairobi huenda yakaahirishwa kutokana na
mkasa wa jumba la Westgate lililovamiwa na magaida wa Al Shabaab, na zaidi ya watu sitini kuuawa.
Mwana mama aliyejeruhiwa akitolewa nje ya jengo hilo ili kufanyiwa matibabu,na kwa nyuma anaonekana mtu ambaye amepoteza maisha kutokana na kupigwa risasi
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa magongo cha Kenya Nashon Randiak anasema shirikisho la kimataifa,FIH, lina wasiwasi kuhusu usalama wa wachezaji mjini Nairobi baada ya magaidi wa Al Shabaab kulivamia jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.
Licha ya Randiak kuwaeleza kwamba hali sasa ni shwari baada ya magaidi wote kuuwa na wanajeshi wa Kenya shirikisho la kimataifa limesema linataka mkuu wa polisi nchini Kenya kuwahakikisha usalama wa wachezaji.
Randiak ameshangazwa na msimamo huo akisema mashambulizi ya magaidi hutokea kote duniani hivyo anashangaa ni kwanini hili la Kenya linachukuliwa ni kama la kipekee..
Mataifa yanayotarajiwa kushiriki kwa wanaume ni Kenya, Ghana na Afrika Kusini na kwa wanawake ni Kenya, Tanzania,Ghana na Afrika Kusini. Timu ya Tanzania ikiongozwa na katibu wa chama cha magongo mkoa wa Dar es salaam Mnonda Magani tayari imeshawasili mjini Nairobi.
katibu mkuu wa chama cha mpira wa magongo mkoa wa Dar es salaam(DRHA)
Mnonda Magani
Timu ambazo zimejiondoa kwa sababu mbali mbali na sio hiyo ya Westgate ni pamoja na Nigeria, Namibia, Misri na Ushelisheli.

WACHEZAJI WA TANZANIA WALIOKWENDA KENYA
Nahodha ni Magreth Eliud,na wachezaji wengine ni Audia Mkucha,Kidawa Selemani,Eva Elias,Miriam Ngomaitara,Mary Muhina,Salome Thomas,Joyce Esabius,Hadija Mohamed,Frola Simbamkole,Mariam Zawad,Leah Shani,Winfida Gowele,Hawa Musa,Happy Ngoko na Sophia Kumpaha.

CHANZO:BBC swahili na jamiinamichezo.blogspot.com

Post a Comment

0 Comments