Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 26,2013 SAA 9:25 USIKU
![]() |
| Robert Lewandoski amethibitisha kuondoka Dortmund ifikapo Januari |
Mshambuliaji wa Borussia
Dortmund Robert Lewandowski ameviambia vyombo vya habari
vya Ujerumani kwamba anatarajia
kuthibitisha kujiunga na Bayern Munich mnamo mwezi Januari.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na vyombo vya habari zaidi duniani kutaka kujiunga na Bayern.
Taarifa zinasema atapewa mkataba wa miaka minne na Bayern - kuanza kwa msimu ujao.Alipoulizwa kama angeweza kuthibitisha hoja ya kujiunga na Bayern mwezi Januari, Lewandowski aliiambia Sport 1: "Ndiyo, kwa sababu siwezi kusaini mkataba mpya mwezi Januari."
Lakini pia Lewandowski alikaliliwa akiiambia Sky Deutschland kwamba anaamini kuwa anaweza hata kuondoka kabla ya majira ya joto.
Kwa sasa, siwezi kusema lolote," aliongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland. "Kwa kawaida, naweza tu kutangaza rasmi mwezi Januari.
"Wakati huu, bado ni mapema mno na itabidi kusubiri kidogo Lakini. Nadhani,naweza kuondoka ikifika Januari."

0 Comments