Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 26,2013 SAA 10:30 ALFAJIRI
Mwisho
wa kumbukumbu: Sanamu ya Michael Jackson ikiondolewa (Jumatano)sanamu iliyokuwa akipendwa na mmiliki wa zamani wa Fulham Mohamed Al Fayed.
Hii ni
(kweli) Ni ule utata wa sanamu ya Michael Jackson nje ya uwanja wa Craven Cottage,kwa maana hiyo sasa ni dhahili shahili
Historia sanamu katika klabu ya Fulham imemalizika siku
ya Jumatano.
Sanamu hiyo ilikuwa nje eneo la mapokezi ya klabu ya Fulham licha ya kashifa zilizowahi kumkuta nyota huyo wa muziki duniani. Mmiliki wa zamani wa klabu hiyo Mohamed Al Fayed aliwahi kuwaambia mashabiki wa Fulham wangeweza 'kwenda jahannamu' kama hawakuipenda sanamu hiyo.
Lakini mmiliki mpya wa klabu hiyo ya London
magharibi Shahid Khan alizungumza kwa
niaba ya mashabiki wa Craven Cottage aliposema 'sasa inatosha', na
alitangaza nia yake ya kuondoa kumbukumbu hiyo ya nyota wa Marekani ambaye
alifariki mwaka 2009.
Ni uamuzi wa boss huyo mpya, uliokuwa umepokelewa kwa furaha na wengine kwa uchungu katika siku ya Jumatano - baada ya hapo klabu ya Fulham iliandika: 'Leo tunasema kwaheri kwa Michael,Shukrani kwa ajili ya kumbukumbu.'
Ujumbe katika akaunti rasmi Instagram ulikuwa akifuatana na video ya sanamu hiyo ikiondolewa kutoka eneo kilo.
Mashabiki
wa Fulham walionekana kuridhika na maamuzi baada ya mmoja wawatumiaji wa Instagram alielezea kama 'siku kubwa kwa Fulham' kabla ya mwingine kuandika: '. Tungeelekea chini ya mto na tumeona hii ni mwisho'
Sanamu hiyo ilikuwa inapendwa sana na Al Fayed, ambao aliwahi kusema: 'Michael Jackson alikuwa ni Legendary wa ukweli,katika muda wake alioutumia ndani ya dunia hii ya kisasa na alikuwa mtu Mashuhuri.
'Alikuwa rafiki yangu,mtu ambaye tulibadilishana kumbukumbu nyingi za furaha na ambaye alikufa kifo cha kutisha.'alisema Al Fayed ambaye ni mmiliki wa zamani wa klabu ya Fulham.
![]() |
| Kifo: Jackson alikufa mwaka 2009 |






0 Comments