Ticker

6/recent/ticker-posts

UMESIKIA HII:MECHI YA YANGA NA AZAM NGAO YA JAMII YAINGIZA MIL 208

Na. Boniface Wambura pamoja na Herman Kihwili,IMEWEKWA AGOSTI 18,2013 SAA 12:40 JIONI
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda Azam bao 1-0.
picha na page ya facebook ya azam fc
Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya
mchango wa kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.
Uwanja sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh. 13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.

Post a Comment

0 Comments