Ticker

6/recent/ticker-posts

MUSSA HASSAN ZUNGU:UCHAWI KATIKA SOKA NI MAZOEZI



Na john Piter. IMEWEKWA AGOSTI 18,2013 SAA 8:30 MCHANA
Chama cha mpira wa miguu kwa mkoa wa Dar es saalam (DRFA) leo kimeendesha semina ya siku moja kwa klabu 11 za Mkoa wa Dar es Salaa zinazoshiriki Ligi Kuu ya na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara ili kuboresha weledi na hatimaye kufanya vizuri.
Mbunge wa Ilala, Mussa Hassan Zungu:alifungua semina badala ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik,kama ilivyotangazwa
Akifungua semina hiyo Mh.Mussa hassan Zungu ambaye ni mbunge wa Ilala,amesema ili kuwa kocha bora lazima ujue sheria zote za
mchezo wa soka ili ulete mafanikio ya soka,
 

Nahodha wa Yanga,Nadir Haroub ‘Canavaro’,naye alihudhulia semina hiyo
Lakini pia zunguwakati wa hutuba yake, aligusia swala la ushirikina katika soka,na kusema, uchawi katika soka hakuna kama hufanyi mazoezi ya kutosha,kamwe hauwezi kufanya chochote katika soka.
Wahudhuliaji wa semina

MOJA YA JAMBO LA KUFURAHISHA NI PALE ILIPOTOLEWA HISTORIA YA MATUMIZI YA  KADI NYEKUNDU NA NJANO KUTUMIKA KATIKA MCHEZO WA SOKA.

Miaka ya nyuma katika kombe la dunia,kulikuwa na mechi kati ya Colombia na Argentina,refa alikuwa muingereza, baada ya kutoelewana kwa Lugha kati ya wachezaji na refa juu ya makosa ambayo yalitolewa pale uwanjani,mpira ulisimama kwa dakika kadhaa.Baada ya mechi kuisha,yule refa akiwa njiani kuelekea nyumbani,barabarani akakutana na taa za kuongozea magari,njano,nyekundu na kijani,ndipo yule refa akapeleka pendekezo kwa Shirikisho la mchezo wa soka duniani (FIFA),kuwa kutokana na kutokuelewana kwa lugha ikaamuliwa kutumika kadi mbili,yaani njano na nyekundu ili kutoa adhabu kwa kadi hizo bila kualibu mchezo.

Post a Comment

0 Comments