Ticker

6/recent/ticker-posts

REAL MADRID YATOA OFA MBILI KWA SPARS ILI WACHAGUE KWA AJILI YA KUMCHUKUA GARETH BALE

Klabu ya Real Madrid imetoa ofa mbili tofauti kawa ajili ya kumchukua winga Gareth Bale na kusuburi kuona klabu ya Tottenham Hotspur inachagua ofa moja.

Gareth Bale:Anataka kufanywa kuwa mchezaji mwenye thamani sana duniani

Imetoa ofa ya kwanza ambayo ni ya €100m (£ 86m) malipo yatayo ambatana na mkataba wa miaka mitatu hadi minne,ambayo itakuwa imeishinda ofa iliyovuka rekodi ya dunia kutoka Manchesta united kwa Cristian Ronaldo ya £80m.

Nyingine ni malipo ambayo itakuwa karibu na £ 70m,ofa hii itakuwa inamfanya kuwa mchezaji wa ghali sana,kwani itamuwezesha kumfanya mchezaji anayelipwa mshahala mkubwa na wenye thamania kuliko Cristian Ronaldo.

Lakini Katika hatua nyingine kocha wa Barcelona  Gerardo Martino imelaani kitendo cha Real Madrid kutaka kumsainisha Gareth Bale kwa ofa hiyo ambayo itavunja rekori ya dunia na kusema uhamisho huo ni ukosefu wa heshima.

Martino amesema: 'Bale ni mchezaji mzuri lakini idadi hiyo ya euros 100m ni kama kuwa na ukosefu wa heshima kwa ajili ya mchezo wa soka  dunia.

Amechukizwa:Gerardo Martino anasema Bale ni mchezaji mzuri lakini idadi hiyo ya euros 100m ni kama kuwa na ukosefu wa heshima kwa ajili ya mchezo wa soka  dunia.

Wakati huo huo Kocha wa Spurs Andre Villas-Boaz hatarajii Bale kuwepo White Hart Lane siku ya kesho katika mchezo dhidi ya Swansea,kwa sababu anaweza   kugeuka kwa sababu ya mpango wake wa kuamia Real Madrid. 

Anawasiwasi: bosi wa Spurs  Andre Villas-Boaz  hafikirii Bale atakuwepo kwa katka  mchezo dhidi ya Swansea

Bale ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 24,amekuwa ana nia ya kujiunga na klabu hiyo ya nchini uhispania ambao wamekuwa katika mazungumza na Spurs juu ya Bale wiki kadhaa sasa.

Bale amejiunga na Spurs kwa kitita cha £10m kutoka Sauthampton mwaka 2007,alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wataalamu wa michezo na chama cha waandishi wa habari za michezo baada ya kufunga mabao 26 msimu uliopita kwa klabu yake hiyo ya White Hart Lane.

 


 

 


 


Post a Comment

0 Comments