Ticker

6/recent/ticker-posts

RASMI:LUIZI GUSTAVO ASAINI NA CLABU YA WOLFSBURG

Mchezaji wa Bayern Munich Luiz Gustavo,amefanikiwa kumwaga wino katika klabu ya Vfl Wolfsburg ya nchini Ujerumani kwa mkataba wa miaka tano.
Gustavo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akingonga vichwa vya habari kuwa yuko mbioni kujiunga na Arsena,lakini ndoto hizo za arsenal zimezimwa rasmi baada ya kutia
saini katika klabu ya Wolfsburg kwa  Mkataba ambao unaaminika ni kati ya euro milioni 15 na 20.
Pigo:Arsene Wenger (kulia)mpaka sasa amemsaini  mchezaji mmoja tu katika majira haya  ya joto
 
wapya waliofika:Mario Gotze(kushoto)na Thiago Alcantara (kulia)  wachezaji waliochaguliwa na Pep Guardiola.                                                                                                    
Kufuatia kuwasili  kwa Thiago Alcantara na Mario Gotze katika
timu ya  Bayern  majira haya ya joto,umuhimu na  nafasi Gustavo imeonekana kupungua msimu huu kwa kiasi kikubwa na Wolfsburg wakawasilisha ofa zao wiki chache zilizopita.
Taifa kwanza: Luiz Gustavo (kulia) alicheza katika mechiya taifa lake la Brazil mapema wiki hii kabla ya kujiunga na Wolfsburg
Luiz Gustavo alijiunga na Bayern akitokea Hoffenheim mnamo Januari 2011, na amaeomba kuihama klabu hiyo ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha  kwanza kwa sababu nafasi zake za kucheza kila mara katika klabu ya Bayern zilikuwa chache msimu uliopita.

Post a Comment

0 Comments