Ticker

6/recent/ticker-posts

NSSF YACHUKUA JUKUMU LA KUPAMBANA NA MALARIA NCHINI.

Na. Herman kihwili,IMEWEKWA AGOSTI 19,2013 SAA 4:47usiku
 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejiunga rasmi katika vita Dhidi ya malaria kama mdau kwa ushilikiano na Wizara ya Afya,shilikisho la sika Afika (CAF) pamoja na taasisi ya United Agaist Malaria (UAM) ambao ni mtando unopiga vita ugonjwa wa malaria ulimwenguni.
Meneja mafao ya matibabu (NSSF) Dr Ali Mtulia
 Akizungumza na waandishi habari leo hii,meneja mafao ya matibabu (NSSF) Dr Ali Mtulia,amesema shirika hilo  litachukua
hatua  zote za  kupambana Malaria  kwa lengo la kuweka mazingira salama ya kazi kwa wafanyakazi,wanachama na waajiri ili kuleta ufanisi kwenye kutoa huduma na uzalishaji na hatimaye kuboresha mafao ya wanachama na watanzania kwa ujumla.
Aidha mtulia ameongeza kuwa,shirika la NSSF ikiungana  na zaidi  ya taasisi tisini 90  barani Afrika na wadau wengine nchini,pia itachukua jukumu la kuchapisha ujumbe wa kutokomeza malaria Kwenye machapisho yote ya shirika na kutoa mada katika mikutano na makongamano yote ya shirika,lakina pia itachapisha nembo ya United Against Malaria katika matangazo yote ya shirika.

Naibu msimamizi wa mpango wa wa kudhibiti MalariaDr.Renata Mandike
Na kwa upande wa serikali iliwakilishwa na  Dr.Renata Mandike,ambaye ni naibu msimamizi wa mpango wa wa kudhibiti Malaria,ambapo amesema kuwa,amefurahishwa na shirika la NSSF kujiunga katika harakati hizo za kupambana ma Malaria,na kuyataka makampuni mengine pia kujitokeza,na kuongeza kuwa, serikali  peke yake haiwezi  kujitosheleza bali pia inatakiwa na wengine waweze kusaidia katika vita hivyo dhidi ya malaria.
 
Balozi wa mpango wa kupambana na malaria nchini, Leodegar Tenga,pia alikuwepo kutoa nasaa.

Pia Dr.Mandike amewataka wananchi kutambua kuwa ugonjwa malaria unatibika na tiba muafaka ipo,lakini pia wananchi  wametakiwa watumie Net zenye dawa maalumu pamoja na kutumia dawa mseto ya malaria,iwapo watapata ugonjwa huo kwani dawa pamoja na neti hizo,zimedhibtishwa rasmi na serikali kwa wanachi kutumia.
Wa kwanza kushoto juu na chini,ni Manager-SA, bi. anna McCartney

Post a Comment

0 Comments