Ticker

6/recent/ticker-posts

GARETH BALE AWASILI HISPANIA

Gareth Bale tayari ameshatia nanga nchini Uhispania kujiandaa kusaini katika klabu ya Real Madrid, lakini Tottenham na viongozi wa Kihispania bado hawajaweka wazi suala la pesa iliyopendekezwa ambayo itavunja rekodi ya dunia.


mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ambaye ana umri wa miaka 24, ameruka kwa ndege binafsi akitokea Malaga na kisha alisafiri kwa teksi mpaka  Marbella, ambapo anatarajiwa kukaa na kufanya 
mazungumzo,na inatarajiwa ndani ya maasa 24 yajayo mchezaji huyo,hatma yake itakuwa imejulikana.

Awali Jamii na Michezo tuliripoti kuwa klabu ya Real Madrid imetoa ofa mbili tofauti kawa ajili ya kumchukua winga Gareth Bale na kusuburi kuona klabu ya Tottenham Hotspur inachagua ofa moja,na ofa ya kwanza ambayo ni ya €100m (£ 86m) malipo yatayo ambatana na mkataba wa miaka mitatu hadi minne,ambayo itakuwa imeishinda ofa iliyovuka rekodi ya dunia kutoka Manchesta united kwa Cristian Ronaldo ya £80m.
Na ofa nyingine ni malipo ambayo itakuwa karibu na £ 70m,ofa hii itakuwa inamfanya kuwa mchezaji wa ghali sana,kwani itamuwezesha kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahala mkubwa na wenye thamania kuliko Cristian Ronaldo.
Jukwaa la kimataifa:Real Madrid wanaonekana kufanya matayarisho ya jukwaa ndani ya Bernabeu,kwa ajili ya kumkaribisha Gareth Bale
Real Madrid inacheza siku ya jumatatu usiku na timu ya Granada katika La Liga,na  Bale anatarajiwa kutambulishwa kabla ya Jumanne.

Post a Comment

0 Comments