Kiungo wa Newcastle  Yohan Cabaye alikataa kucheza na timu yake ambayo ilitoka sare ya bila kufungana wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani na timu ya West Ham United siku ya jumamosi kufuatia timu ya Arsenal kuwa tayari kumchukua mchezaji huyo kwa kitita cha £10.

kaweka mgoma baridi,kisa uhamisho wake kwenda Arsenal

Michezaji huyo wa kimataifa wa  Ufaransa pia alikosa mechi ya Jumatatu ambayo Newcastle walipigwa mabao 4 kwa 0 na manchester city na sababu inaelezwa ni baada  harakati za Arsenal.

"Ni rahisi sana - tunahitaji kutatua hii hali," alisema Pardew."Tunahitaji kukutana na yeye mwenyewe kwa nafasi yake, kama yeye anakaa, na kama  yeye hatakaa tunahitaji kujua usawa mzuri." Kuna haja ya kuwa na biashara kutoka kwetu, kuwa na biashara ni haki kwa Newcastle na  mashabiki wetu, kupata nafasi ambayo kweli wanataka kuamini katika timu,haiwezekani  kwa klabu kubwa kuwa na  wachezaji wengi  na kugombana,alisema Pardew.

Atatua kweli Arsenal?

Cabaye imecheza mechi 73 katika klabu yake yaNewcastle tangu alipojiunga kutoka Lille  Juni 2011.

dirisha la usajili linafungwa siku ya jumatatu ya septemba 2 majira ya saa  - 23:00 BST