Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA 07,SEPT.2018 SAA 12:50 JIONI
...>>>.....
Mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi
Simba, kesho watacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard
kutoka
nchini Kenya, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mchezo wa mzunguuko wa
tatu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara utakaowakutanisha na Ndanda FC mjini
Mtwara mwishoni mwa juma lijalo.
Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya SImba Haji
Sunday Manara amesema mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es
salaam mishale ya saa kumi na mbili jioni.
Mbali na mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki
utakaochezwa kesho uwanja wa taifa Dar es salaam, Haji Manara akatumia nafasi
ya mkutano na waandishi wa habari kuwakumbusha wanachama wa klabu ya Simba
kutumia muda uliopo kuchukua fomu za kuwnaia nafasi mbalimbali za uongozi wa
klabu hiyo.
BOFYA CHINI KUSIKILIZA

0 Comments