Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.01.2018 SAA 11:52 JIONI
BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia Rapa
Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ kwa muda wa miezi sita
kutojihusisha na sanaa ya
muziki kutokana na kutotii agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo lililomtaka kubadilisha maudhui ya wimbo wake wa KIBAMIA.
Kutokana na wimbo huo ambao Roma amewashirikisha
wasanii wenzake, Stamina na Maua Sama, Basata walimuita na kumweleza arekebishe
maudhui ya wimbo lakini inasemekana hakutekeleza agizo hilo hivyo BASATA
wameamua kumfungia.
Maamuzi ya kufungiwa kwa msanii huyo yametangazwa
na naibu waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Julianza Shoza
alipozungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam.
Katika hatua nyingine Wiziri wa
habari, sanaa, utamaduni na michezo imempa onyo msanii Nay wa Mitego baada ya kufanya naye mazungumzo,ambapo Nay wa Mitego amepewa maelekezo ya kufanya
mabadiliko katika moja ya nyimbo zake ambazo zina maneno tata.
Ney Wa Mitego alikufanya mazungumzo na viongozi wa BASATA
pamoja na wizara ya habari, usanii na michezo, na kuahidi kufanya
marekebisho ya baadhi ya maneno tata katika wimbi wake wa Mikono Juu.
VIDEO
0 Comments