Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.NOV 11.2016 SAA 01:11 USIKU
Timu ya Mpira wa Miguu ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro kutoka
Kampuni ya Bia Tanzania inatarajiwa
kuondoka leo Ijumaa saa 7.15 mchana Novemba 11, mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
kuondoka leo Ijumaa saa 7.15 mchana Novemba 11, mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika
jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya
mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni: Makipa
Deogratius Munishi na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael
Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.
Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim,
Jonas Mkude na Muzamiru Yassin na wale wa pembeni ni ni Shiza Kichuya,
Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuluaji ni Ibrahim Ajib, John
Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda
.
Mchezo huu utakuwa na faida zaidi kwa Tanzania
kama ikiwafunga Wazimbabwe kwa kuwa itaongeza alama za nyongeza kwa
kushinda ugenini.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima
viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika
nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora.
Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji
anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta
anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu
nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani
ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38)
na Ghana (45).
0 Comments